Tuesday, August 8, 2017

KUMBE HELA ZINAPATIKANA KIURAHISI HIVI? ACHANA NA "MAGUFULI KABANA"

2 comments
Zifahamu njia 5 kali za kupata hela ndani ya masaa machache na utakuwa mmoja wa mashihidi walioleta ushuhuda kwangu. Njia hizi ni njia ambazo kabla ya kuzileta kwenu zimethibitishwa na kuhakikishwa na watu wengi kuwa ni za kweli na zinaweza kukufanya usisahau shida nyingi za kimaisha. Usininukuu vibaya ila unawez ukawa BILIONEA. Furahia maisha


Kwa kusema hivyo najua wengi wameshaanza kuwaza ujasiriamali au ufanya biashara vichwani mwao lah, Kwani tajiri namba moja duniani,BILL GATES ni mjasiriamali au mfanya biashara? kunatofauti kubwa kati ya vitu hivyo viwili...angalia chini
                       "A businessman walks on the defined path, but              an entrepreneur believes in making his own path, which becomes a guideline for other businessmen. Most of the people have a misconception that the terms businessman and entrepreneur, carry the same meaning, due to which they use them interchangeably."  Soma zaidi: UJASIRIAMALI NA BIASHARA


HIZI NDIZO NJIA 5 ZA KUPIGA HELA MTANDAONI

1.FUNGUA YOUTUBE CHANNEL UONE MAAJABU
Youtube ni mtandao unaohusiana na videos kwa kutuma au kuangali. Mwaka ulioisha Felix kjellberg CHEKI alipata takribani dollar milioni 15.5 kwa ajir ya youtube tu.Ili uvune pesa nyingi juu ya mtandao huu unatakiwa kufungua channel ambayo hiyo utatumia kama sehemu yako ya kutuma au ku-upload videos. Ili kutengeneza pesa kwa Youtube, kikubwa unatakiwa kuwa na email address ambayo utatumia hiyo kufungulia channel yako ya Youtube ambayo mtandao huu upo chini ya kampuni ya Google kwa maana hiyo kufungua kwako channel ya Youtube kutakufanya uwe kama umeajiriwa na Google. Jaribu leo uone mafanikio ya youtube.

2.TUMIA WEBSITES ZINAZOLIPA DOLA
Takwimu zinaonyesha asilimia 11 ya watanzania mwaka 2015 walikuwa wanatumia smartphones.waaoh,nidhahiri kabisa mwaka huu 2017 asilimia hiyo itakuwa imeongezeka.Sasa kwann usitumia simu yako iyo kupata kipato.Tembelea web zifuatazo kupata mpunga kiulaiiiniiii.

   a) SwagBucks
 swagbucks ni mtandao maarufu sana duniani ambao ukiutembelea na kujiunga tu,unapata dollar 5.Mbali na hapo,ukifanya shughuli nyingine kama searching,surveying...wazungu wanasema unapata extra cash..jaribu uone
   b)websites nyingine ni kama
-InboxDollars.com
-Globaltestmarket Ingia hapa

3. NJIA NYINGINE MAARUFU NI KUTUMIA AMAZON AFFILIATES
Amazon ni mtandao maarufu sana unaomilikiwa na tajiri aliyeshika namba moja mwaka huu JEFF BEZOS.Kazi kubwa ya AMAZONI ni kuuza bidhaa mbali mbali ulimwenguni kote.

Sasa wewe kama amazon affiliates unachotakiwa kufanya baada ya kujiunga ni kuomba waweke matangazo yao kwenye  website au blog yako.Sasa mtu yeyote akinunua bidhaa kupitia mtandao wako basi unapata faida kubwa na malipo yao sio mabaya.

4.TENGENEZA BLOG UONE MAFANIKIO
Watu wengi wamekuwa wakichukulia poa swala la kuwa na blog.Kweli ni changamoto kwa sababu inahitaji muda na kujitoa pia inahitaji iwe ni kazi unayoipenda.  Mwaka jana Huffington aliweza kupata kiasi cha dolla milioni 14 ambayo ni sawa na Tsh 3220000000000.

Anzisha blog yako kwa kutumia BLOGGER au WORDPRESS halafu itengeneze vizuri kwa msaada wa matengenezo TUWASILIANE.
Kuhusu blog Tembelea MITAANI FORUM

5.UZA BIDHAA ZAKO ONLINE
Kama hujawahi jaribu basi hii ni dili bomba.Kama una bidhaa zako tembelea website MITAANI FORUM
Read More

Friday, August 4, 2017

TAJIRI RICHIE NORTON YAMKUTA MAZITO,MAOMBI YENU

Leave a Comment
Mwandishi maarufu wa kitabu maarufu cha "power of starting something stupid" na anayeongoza kwa Download ndani ya Amazon "Resumes are dead and what to do about it" na baba wa watoto watano (Mmoja alifariki akiwa na wiki kumi akiumwa dondakoo) yamekuta mazito baada ya mtoto wake wa miaka 10(jina halijajulikana) kugongwa vibaya na gari aina ya SUV.

Taarifa zinaonyesha mpka sasa mtoto huyo yupo katika chumba maalumu(ICU) akiendelea na matibabu.Baba yake,mr Norton amesema haya kwenye akaunti yake ya Linkedin.

Read More

Thursday, August 3, 2017

ISOME HII MPYA YA NACTE

Leave a Comment


TAARIFA KWA UMMA





 





KUHUSU KUHAMA KWA OFISI YA NACTE KANDA YA KASKAZINI





 



Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE), linapenda kuuhabarisha Umma na wadau wa Elimu nchini hasa wa kanda ya Kaskazini ya kwamba, ofisi ya baraza ya kanda ya kaskazini imehamia katika jengo jipya la NSSF COMMERCIAL COMPLEX (MAFAO HOUSE) ghorofa ya nane (8), jengo hili lipo katika barabara ya Old Moshi, Plot No. 1. Karibu na New Arusha Hotel kuelekea Kibo Palace Hotel.

 

Kabla ya kuhama ofisi hizo zilikuwa katika majengo yaArusha Technical College (ATC) Chumba namba nne (4), karibu na njia panda ya barabara ya kuelekea Nairobi (Namanga Road) na ile inayotoka Moshi.

 

Kwa maelezo zaidi, wasiliana na Ofisi zetu za Kanda ya Kaskazini kwa anuani zifuatazo;-

 

NACTE Northern Zone

P.o. Box 14333 Arusha,

Mobile: 0658444556/57

Email:northern.zone@nacte.go.tz

 

 

IMETOLEWA NA;





KITENGO CHA HABARI MAWASILIANO





BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)





3/08/2017




Read More

Wednesday, August 2, 2017

SEHEMU YA KWANZA: HAKUNA ANACHOKITAKA MWANAMKE ZAIDI YA HIKI HAPA CHINI

Leave a Comment
Kuna mengi yanatokea kwenye jamii haswa kwenye swala zima la mahusiano. Mahusiano yamekuwa na pande mbili yani upande wa chumvi na upande wa sukari na kupelekea watu kuwa na mitazamo tofauti juu ya mahusiano.Yapo mengi yanasemwa juu ya hili na pande kuu mbili yaani wanawake na wanaume wamekuwa wakizozana kuwa ni nani chanzi cha sintofahamu kwenye mahusisano au ni nani chanzo kikuu cha faraja kwenye mahusiano.Hakuna shida,Leo tutapata ufumbuzi juu ya hili..Ngoja tuangalie kwanza yafuatayo.

Katika sehemu hii ya kwanza tutazungumzia mambo makubwa mawili yanayomuhusu mwanamke,ninaposema mwanamke namaanisha yule aliyefikia umri wa kuwa kwenye mahusiano japo wazungu wanasema "Love knows no age" lakini katika jamii zetu za kiafrika yamkini hilo sio la kweli.Mambo haya makuu mawili tutakayoyazungumzia leo ni yale ambayo mwanamke yeyote anayahitaji na angependa yule muhusiano wake ayafahamu na ayatimize....

                       1) LUGHA YA MWANAMKE

Ili mahusiano yaweze kudumu na kuendelea  lazima tufahamu lugha kuu ya mwanamke.Wanawake wanawake lugha yao kuu ni DUARA,hii namaanisha wanapenda kuongea kwenye duara..subiri utaelewa.Kama ni mwnamke unasoma na unathibitisha hili ninalosema naomba komenti yako na nyongeza uliyonayo.

Ninavosema duara namaanisha kuwa wanawake wanapenda kuzunguka kwenye maongezi yao yawe ya mahusiano au lah. Twende sawa,mwanamke kama anataka kitu A lazima aanzie mbali,yaani ni kama ndege inapotaka kutua uwanjani lazima izunguke kwanza uwanja ndo itue,kwahiyo kama hujui ndege inavyotua utawaza labda inataka kupaa.

Mara nyingi mwanamke anachoongea mara ya kwanza kwenye mahusiano sicho anacho maanisha.Mfano,mwanamke anaweza akakwambia sihitaji kitu Fulani wakati au mfano mzuri ni pale mnapokuwa na familia na watoto alafu labda watoto wakawa wasumbufu na baba upo kimya,mwanamke huwa anatafuta ni jinsi gani ataweze kufikisha taarifa kwako,wengi wao wanaweza kukwambia,baba naniii hivi unaangaliaga madaftari ya watoto?lakini lengi ni kukwambia kuwa watoto wasumbufu.

Kwa hiyo kama wanaume lazima tufahamu lugha kuu ya wanawake wetu ambayo wao wanaamini tunaijua yamkini wanaume wengi imekuwa ikitusumbua sana. Kwa hiyo njia ya kwanza ya kuponya mahusiani ni kutambua lugha ya mwanamke anayoitumia,hii itatuwezesha kutibu matatizo mengi sana na  kuwa na mahusiano mazuri yenye Amani.

                           2) UPENDO "AFFECTION" NOT JUST "LOVE"

Hiki ndicho kitu kikubwa cha pile tutakachokizungumzia katika sehemu ya pili abacho kinauhusu kwa kiingereza "affection". Affection sio upendo wa kawaida ule wa I LOVE YOU ni zaid ya hicho..
TUKUTANE SEHEMU YA PILI.

Read More

Tuesday, August 1, 2017

KICHWA CHAKO,HALMASHAURI YAKO

2 comments
Katika maisha haya tunayoishi,maamuzi ni jambo la msingi sana ambalo ukilifanya kwa usahii unaweza kuona matunda yake lakini vile vile ukifnya namna gani vipi lazima uje kujuta.


Ujue kuna watu wa aina kama tatu hivii

a) Hawa ni watu ambao huwa hawanaga maamuzi,wao wanafuata kile ambacho wengi wanakipenda,na wengine wakijifunika kwenye mwamvuli wa demokrasia. Watu hawa huwa hawafanikiwagi kwa sababu anakuwa hana msingi,na nyumba iliyojengwa nje ya msingi sio nyumba.Vitabu vya dini vinasema

b) hawa wa aina ya pili ni wale wanaofanya jambo kumfurahisha fulani na sio kwa mapenzi yao.watu hawa huwa kwenye huzuni sehemu kubwa ya maisha yao na mafanikio kwao hasa ya mioyo yao huwa ni duni sana wengine mpaka hufikia kujiita wana "gundu"

c) Hawa ni wale ambao wazungu huwaita "One man army" yaani ikimaanisha jeshi la mtu mmoja. Hawa huwa husimamia misimamo yao na huamini halmashauri za vichwa vyao kuliko kitu kingine chochote yani. Mtu wa hivi hata kama mia wanekibali au wamepinga kitu,yeye huwa anaweza akaenda kinyume nao alimradi tu awe anaamini kile alichotumwa na halmashauri yake.

Na hiyo "C" ndiyo siri ya mafanikio.Simamia misimamo yako,usikubaki kuyumbishwa na mtu wala kitu. Wazungu hupendelea kusema "Follow your brain but take your heart with you" Tutaizungumzia siku ingine iyo.

Je unataka kujua jinsi ya kusimamia misimamo yako?
Read More

HAYA NDIO MAMBO 6 YA AJABU YA JUA

Leave a Comment
Jua ni moja ya nyota kubwa kabisa ambayo inakadiriwa kuwako kwa zaidi ya miaka bilion 4.5. Pia jua ni kitovu na sehemu ya katikati katika mfumo mzima wa sayari.

Jua hili pia ni chanzo cha nishati yote ambayo unaiona duniani.Hii ikiwemo ile ya umeme na hata nishati itokanayo na mimea.  ambacho kinatusaidia sisi pamoja na wanyama wengine kwa maisha ya kila siku.
MAAJABU SITA USIYO YAJUA YA JUA

1.Jua kwa kiingereza "sun" ni jina lenye asili ya neno la kiingereza "sunne" kutoka katika kiingereza cha zamani sana.

2. Jua lina usumaku "magnetic field"  kama sumaku ambapo pande zake mbili (North and south) hupinduka kila baada ya miaka 11.

3. Photosphere ambayo sehemu ya katikati ya jua,ndiyo sehemu ambayo inatoa joto ambalo ndilo huwa mwanga "light" ambao unatufikia Duniani.kutokana na umbali kutoka kwenye photosphere ambao  ni mile 300 ,mwanga wa jua hutumia zaidi ya dakika 8 kufika duniani.
4. Sehemu ya nje ya jua " corona" ndiyo yenye joto zaidi kulinganisha na sehemu ya ndani ya jua photosphere inayotoa 5500 centigredi kulinganisha na corona yenye jotk zaidi ya degree milioni 3 kulinganisha na corona.

5.Kipenyo cha jua ni kutoka katikati mpaka kwenye ukingo nj 864,575.9 miles na kipenyo cha jua mpaka kwenye dunia ni miles 92.96.Uzito wa jua ni zaidi ya mara 330,000 ya ule wa dunia.

6.Viumbe vyote duniani vinahitaji jua ili viendelee na maisha.Mimea ya kijana na isiyo ya kijani inahitaji jua ilikuweza kujitengenezea chakula chake yenyewe (photosynthesis),ambapo mimea hii sisi huitumia kwa chakula
 
Read More