Wednesday, August 2, 2017

SEHEMU YA KWANZA: HAKUNA ANACHOKITAKA MWANAMKE ZAIDI YA HIKI HAPA CHINI

Leave a Comment
Kuna mengi yanatokea kwenye jamii haswa kwenye swala zima la mahusiano. Mahusiano yamekuwa na pande mbili yani upande wa chumvi na upande wa sukari na kupelekea watu kuwa na mitazamo tofauti juu ya mahusiano.Yapo mengi yanasemwa juu ya hili na pande kuu mbili yaani wanawake na wanaume wamekuwa wakizozana kuwa ni nani chanzi cha sintofahamu kwenye mahusisano au ni nani chanzo kikuu cha faraja kwenye mahusiano.Hakuna shida,Leo tutapata ufumbuzi juu ya hili..Ngoja tuangalie kwanza yafuatayo.

Katika sehemu hii ya kwanza tutazungumzia mambo makubwa mawili yanayomuhusu mwanamke,ninaposema mwanamke namaanisha yule aliyefikia umri wa kuwa kwenye mahusiano japo wazungu wanasema "Love knows no age" lakini katika jamii zetu za kiafrika yamkini hilo sio la kweli.Mambo haya makuu mawili tutakayoyazungumzia leo ni yale ambayo mwanamke yeyote anayahitaji na angependa yule muhusiano wake ayafahamu na ayatimize....

                       1) LUGHA YA MWANAMKE

Ili mahusiano yaweze kudumu na kuendelea  lazima tufahamu lugha kuu ya mwanamke.Wanawake wanawake lugha yao kuu ni DUARA,hii namaanisha wanapenda kuongea kwenye duara..subiri utaelewa.Kama ni mwnamke unasoma na unathibitisha hili ninalosema naomba komenti yako na nyongeza uliyonayo.

Ninavosema duara namaanisha kuwa wanawake wanapenda kuzunguka kwenye maongezi yao yawe ya mahusiano au lah. Twende sawa,mwanamke kama anataka kitu A lazima aanzie mbali,yaani ni kama ndege inapotaka kutua uwanjani lazima izunguke kwanza uwanja ndo itue,kwahiyo kama hujui ndege inavyotua utawaza labda inataka kupaa.

Mara nyingi mwanamke anachoongea mara ya kwanza kwenye mahusiano sicho anacho maanisha.Mfano,mwanamke anaweza akakwambia sihitaji kitu Fulani wakati au mfano mzuri ni pale mnapokuwa na familia na watoto alafu labda watoto wakawa wasumbufu na baba upo kimya,mwanamke huwa anatafuta ni jinsi gani ataweze kufikisha taarifa kwako,wengi wao wanaweza kukwambia,baba naniii hivi unaangaliaga madaftari ya watoto?lakini lengi ni kukwambia kuwa watoto wasumbufu.

Kwa hiyo kama wanaume lazima tufahamu lugha kuu ya wanawake wetu ambayo wao wanaamini tunaijua yamkini wanaume wengi imekuwa ikitusumbua sana. Kwa hiyo njia ya kwanza ya kuponya mahusiani ni kutambua lugha ya mwanamke anayoitumia,hii itatuwezesha kutibu matatizo mengi sana na  kuwa na mahusiano mazuri yenye Amani.

                           2) UPENDO "AFFECTION" NOT JUST "LOVE"

Hiki ndicho kitu kikubwa cha pile tutakachokizungumzia katika sehemu ya pili abacho kinauhusu kwa kiingereza "affection". Affection sio upendo wa kawaida ule wa I LOVE YOU ni zaid ya hicho..
TUKUTANE SEHEMU YA PILI.

Kama umeipenda,Tumia sekunde 5 kuishare na kukomenti

0 comments:

Post a Comment