Tuesday, August 1, 2017

KICHWA CHAKO,HALMASHAURI YAKO

2 comments
Katika maisha haya tunayoishi,maamuzi ni jambo la msingi sana ambalo ukilifanya kwa usahii unaweza kuona matunda yake lakini vile vile ukifnya namna gani vipi lazima uje kujuta.


Ujue kuna watu wa aina kama tatu hivii

a) Hawa ni watu ambao huwa hawanaga maamuzi,wao wanafuata kile ambacho wengi wanakipenda,na wengine wakijifunika kwenye mwamvuli wa demokrasia. Watu hawa huwa hawafanikiwagi kwa sababu anakuwa hana msingi,na nyumba iliyojengwa nje ya msingi sio nyumba.Vitabu vya dini vinasema

b) hawa wa aina ya pili ni wale wanaofanya jambo kumfurahisha fulani na sio kwa mapenzi yao.watu hawa huwa kwenye huzuni sehemu kubwa ya maisha yao na mafanikio kwao hasa ya mioyo yao huwa ni duni sana wengine mpaka hufikia kujiita wana "gundu"

c) Hawa ni wale ambao wazungu huwaita "One man army" yaani ikimaanisha jeshi la mtu mmoja. Hawa huwa husimamia misimamo yao na huamini halmashauri za vichwa vyao kuliko kitu kingine chochote yani. Mtu wa hivi hata kama mia wanekibali au wamepinga kitu,yeye huwa anaweza akaenda kinyume nao alimradi tu awe anaamini kile alichotumwa na halmashauri yake.

Na hiyo "C" ndiyo siri ya mafanikio.Simamia misimamo yako,usikubaki kuyumbishwa na mtu wala kitu. Wazungu hupendelea kusema "Follow your brain but take your heart with you" Tutaizungumzia siku ingine iyo.

Je unataka kujua jinsi ya kusimamia misimamo yako?
Kama umeipenda,Tumia sekunde 5 kuishare na kukomenti

2 comments:

  1. That is true Nuruel .....must use our brains for our lifetime successful

    ReplyDelete
    Replies
    1. Karibu sana na uwe mfano kwa wenzako. Endelea kutembelea blogu yetu

      Delete